Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo huu hiyo starter nashida nayo leo hii, ikichelewa basi kasho niipate.
Nataka mtumba kutoka Japan au Dubai sio used bongo, pia kama unayo mpya, kama kuna mtu anazo zote mbili mpya na mtumba naomba aje hapa na picha tufanye biashara.
Wauzaji wote hakikisha umesajiliwa na kutambulika yaani verified Members only.
@tokyo-used-parts Niko Katoro nimekwama hapa kama unayo serious naomba picha.
@jonson-john Parefu sana mkuu,kula 300k nifunge zero km hiyo.
Asante next time,hii bei yake sikupunguzi hata mia mkuu.
Kila Tarehe 27 Mwisho wa mwezi,tunapakia Container kutoka Japan kwenda Dar✅ Lipia mzigo wako mapema week moja kabla ya mzigo kuondo.✅✅👍💪🙏🏿
Yes hii ni yenyewe ,fanya 200,000 tumalize hii biashara unitumie nifunge.
@tokyo-used-parts @admin @Digxam nimekubalina na @tokyo-used-parts kuniuzia Starter kwa bei ya 130,000 Tsh hii bei ni pamoja na ghrama ya kutuma mzigo huu kwanjia ya Basi Katoro leo hii.Malipo tayari nimefanya kwenye E-wallet yake.Kama kutatokea changamoto yoyote baada ya kupokea mzigo nitawajulisha @admin
Asante sana kwa huduma hii Mungu awabariki wote.
@jensen Asante sana,mzigo wako uko mjiani kuelekea Urafiki Ubungo,tukutane hapa kesho baada ya kuupokea.
@tokyo-used-parts Hakikisha unamtumia na receipt ya IFD kwenye mzigo wake.
@digxam Tayari nimemuwekea kwenye mzigo wake,akipokea atasema mwenyewe.
Mzigo umefika tayari nimefunga Asante sana