Utawala wa Rais Donald Trump umeamua kusitisha usambazaji wa dawa muhimu za kuokoa maisha kwa magonjwa ya VVU, malaria, na kifua kikuu, pamoja na vifaa vya matibabu kwa watoto wachanga, katika nchi zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
Hatua hiyo ni sehemu ya kusimamisha kwa muda msaada wa Marekani duniani kote ili kupitia upya programu hizo. Taarifa hiyo imetolewa kwa wakandarasi na washirika wanaofanya kazi na USAID, ikiwa ni pamoja na kampuni ya Chemonics, ambayo inashirikiana na USAID kusambaza dawa hizo muhimu duniani kote.
Sasa mbona kama anakomoa yule mwamba simkubali kwanza mambo yake yake ipo tofauti na binadamu wengine