Kimsingi mafanikio yako huja pale unapojua ulipo toka na unapo kwenda, kwasababu itakusaidia kujua kama umekwama, au unasonga taratibu, au unakwenda kwa kasi inayofaa.
katika kujitahimini ni lazima uanze kuangalia wewe binafsi umeanza lini kutafuta pesa au kukimbizia ndoto yako, kimsingi anza kujiangalia tangu ulipo maliza shule na kuingia mtaani rasmi, kwasababu watu wengi tunaanza rasmi kutafuta pesa baada ya kumaliza shule iwe shule y msingi, sekondari, au chuo.
kimsingi pale tuna anza kujichunguza ndipo tunapo jua kwamba tnakwendaje katika kasi ya kufikia malengo yako.
lakini pia unaweza ukajifanyia tathimini tokea kipindi ulicho tambua lengo lako kwa au kuelewa kusudi lako, ndipo uanze kupima kasi yako ya kufikia mafanikio yako, angalia kwa kipindi gani umeanza kutafuta kutimiza lengo lako katika maisha.
siyo siri ukiona huridhishwi na kasi yako, anza kujipanga upya namna ya kufikia malengo yako anza kutafuta njia sahihi ya kufika kwa haraka kule unako pata na kuleta aina ya matokeo unayo stahili.
zifuatazo ni baadhi ya mbinu unazoweza ukazitumia katika kufikia malengo yako,
hakikisha unakuwa na malengo ya kila siku kuelekea ndoto yako, jambo linalokufanya mpaka leo uwe bado kutumiza malengo yako ni kutokana na kupoteza muda mwingi bila ya kuwekeza kwenye ndoto yako. anza sasa kupanga kujieleimisha kupitia ndoto zako, wekeza muda mwingi kwenye kutafakari na kufanya vitu vinavyo kuskuma au kufanya kufikia malengo.
jifunze kuvumilia mpaka ufanikiwe, baadhi ya sababu zinazo chelewesha mafanikio yetu ni kukata tamaa katikati na kupoteza muda mwingi tukijilaumu na kuumia moyoni, alafu baadae tena tunaanza baada ya mwaka au miezi kadhaa, kwasababu zingine tena tunajikita kwenye lile jambo kwasababu imani yetu ni kubwa na kuona namna ya kujifunza kupitia makosa. na ndio maana unaambiwa hutakiwi kukata tamaa hold on mpaka ufanikiwe.
matumizi ya pesa, pesa yako inamchango mkubwa sanaa katika kutimiza ndoto yako, ukiwa na matumzi mabovu ya pesa yako ni lazima utachelewa kufanikiwa. kuwa bahiri tumia pesa kwenye mambo ya msingi tu, na jitahidi kupunguza matumizi ya anasa.
ishi maisha ya kujiheshimu, usikubali kuishi maisha ambayo watu watakuwa wanakudharau hakikisha unaboresha maisha yako yote, boresha muonekano wako, kuwa na muonekano wa kuaminika, kuwa na muonekano wa kuvutia kwa kuwa msafi na mwenye tija katika jamii.
Wangapi wangependa kujifunza ujasiriamali tukutane kwenye comments section.Naomba kila mtu share kwenye mitanda yakijamii itatusaidia kupata watu wengi bilakuchelewa kuanza mafunzo yetu.
Hii elimu ya ujasiriamali naitoa bure kupitia kwenye jukwa hili lakini itategemea na muitikio wa watu kuwa na kiu ya kujifunza mbinu mpya jinsi ya kukabilina na tatizo la ajira.
Niko Tayari
Karibu masai
Niko Tayari kujiunga na ujasiriamali I see.
Darasa linaanza lini chief?