1: UWAKALA WA MITANDAO YA CM
M-pesa
Tigopesa
Airtel money
Halopesa
2: Duka la maziwa fresh+mtindi + juice fresh
3: Banda la chipsi + vinywaji
ANGALAU KWA MWEZI NIINGIZE 300,000 TU
(300,000)
Banda la chips pasua kichwa, inventories nyingi tena makorokoro madogo madogo. Usimamizi mkali na mauzo yanaweza onekana ila faida ikakosa au ukawa unajipunja kipimo. Kwanza mwanamke na biashara ya chips utatumia nguvu nyingi kwa huo mtaji.
Hiyo ya transactions huwa naona ni ya kukuzia awareness tu kama una biashara nyingine hapohapo. As long as hulipi kodi kuanzisha hiyo biashara, otherwise gharama za uendeshaji ni kubwa huku faida ni kidogo na chances za hasara ni kubwa hasa kwa unayeanza. Ukiitaka hiyo uwe na uwakala wa mabenki pia.
Hiyo ya maziwa angalau. Ila zote tatu zinategemea location zaidi. Location ni muhimu kuliko maelezo
Nianze kwa kukutakia kila la heri. Naona kama hizi biashara ni common sana kwa Dar, hivyo basi unatakiwa upate location nzuri sana. Ukishindwa kupata location nzuri basi jaribu kutafuta biashara nyingine.
Kwakua umelimit hizo ideas tatu then mi nasema stick na ya tatu
Daaah sijui nisemeje ila nipo tayari kukupa sapport kwa kazi zote ulizo orodhesha hapo maana nishawahi kufanya.
Hivo ukianza tu kama utahitaji kijana ambaye mwaminifu na anajitambua nipo hapa na nitafanya kwa ubunifu wa hali ya juu aisee.
Sapport pia kwenye capital ipo ila tu kama location ikawa nzuri nipo tayari kabisa
Ishi na namba 3... Hafu unaweza jumlisha na namba 2 kidogo kdoogo... achana na mpesa
Mchawi kuanza. Mtoa huduma alieanza leo analipwa commission tofauti na alieanza miaka 10 iliopita ata kama kwa siku wametoa huduma sawa.
Hiyo ya M pesa mchawi location tu na kwa wadada naona inawafaa sana haina mishkeli mingi.
Japo wadau wameipiga vita sana ila kwa mimi ningeichagua hiyo.
Chipsi zina mambo mengi na ni lazima utafute mtu wa kukusaidia, uendeshaji wake ni gharama lakini pia inahitaji sana umchunge mfanyakazi wako, tofauti na mpesa ambayo unaifanya mwenyewe.
Hizi biashara hazitomlipa sababu ya mtaji wake. Mfano location nzuri ya kuweka transactions unakuta inalipiwa kodi sio chini ya 150,000 kwa mwezi na unalipia miezi sita na ya udalali hapo.
Hiyo ni 1M imekata. Hujaweka zile meza ndani na vioo na mashine za mabenki ambazo zinalipiwa hadi 1M kwa CRDB na NMB. Then ndio uje kwenye float.
Ila kati ya zote maziwa angalau
Uza simu (Smartphone) kwa njia ya mkopo
Fungua kiyepe point kama umeona location nzuri.
Biashara ya uwakala inaenda kufa au? Mboni watu wanaipiga madongo sana?
Asante sana kwa ushauri mzuri nitaufanyia kazi