SIMULIZI - PENZI LA...
 
Notifications
Clear all

Breaking News SIMULIZI - PENZI LA MUUWAJI.

7
Topic starter
image

 

SIMULIZI - PENZI LA MUUWAJI.
MWANDISHI-FAHAD JINNI
EMAIL - fahadjinni01@gmail.com
FB,IG, TIKTOK - FAHAD JINNI
NO: +255657192690

SEHEMU YA 8

TULIPOISHIA
Akapata wazo la kufungua miradi kadhaa ya kumuingizia hela, akawaza kufungua duka la simu ,duka la nguo na Supermarket.
Kwenye kufungua miradi hakua na shaka kwa sababu alikua ana hela nyingi tu na bado alikua na uwezo wa kuingiza zaidi ya million 10 kwa siku.
Akaingia mitandaoni kutafuta madalali , akampata akashindwa kumpigia kutokana bado ilikua ni usiku akamuandikia ujumbe kua anahitaji sehemu tatu za kufungua supermarket na fremu nne za kufungua maduka ya nguo na mbili kwa ajili ya maduka ya simu alitaka ndani ya muda mfupi ziwe zimepatikana.
Baada ya hapo akaenda kwenye chumba chake cha siri akaingia kwenye system ya serikali akajaza maelezo yanayomuhusu yeye kua ni mfanyabiashara ili hata akifatiliwa na maryam asitiliwe mashaka kisha akamtumia ujumbe maryam ya kumtakia usiku mwema kisha akamua kujipumzisha.

*********

Songa Nayo....

Maryam alifika nyumbani kwake akiwa na furaha isiyo na kifani, kila muda alikua akimuwaza Fahad na kuona kweli alikua ni mwanaume sahihi kwake , kwanza hakuonekana kua na mambo mengi pia alikua ni mzuri kimuonekano hadi kitandani alikua anamuweza hakuona sababu ya kuachana na Fahad japo hakutaka kumpa uaminifu kwa asilimia kubwa kutokana bado penzi lao ndio kwanza lilikua linaanza kuchipua. Alienda kujimwagia kisha kuingia kwenye chumba chake ambacho hukifanya kama ofisi yake ya nyumbani.
Aliendelea kufanya kazi zake za kiserikali kama kupitia mafaili ya baadhi za kesi.

*****
Simu ya Fahad iliita ila alikua katika usingizi akatazama kioo cha simu na kuona ni yule dalali aliemtumia ujumbe kwa ajili ya kufungua biashara zake akaipokea na kuiweka sikioni.
"Habari yako kiongozi" aliongea yule dalali alionekana ni mtu mzima kiasi.
"Salama nambie" alijibu Fahad kwa sauti ya uvivu iliyochanganywa na usingizi
"Aah nilikuta ujumbe wako ila kwa bahati nzuri umefika kwenye wakati uliokua sahihi , kuna mzungu alikua na super market zake nne alikua anaziuza anataka kurudi nchini kwao marekani, na pia kuna mchaga ana maduka ya nguo kariakoo matatu nguo za kike za kiume na za watoto hayo ni maduka matatu yaliyokamilika alikua anauza kwa sababu anadaiwa na benki , kwa hio hapo itakua bado duka moja ndio nalifatilia na kuhusu fremu za kuuza simu pia umepata ila zipo kariakoo pale mbili na makumbusho ipo moja kwa hio utaangalia ulitaka supermaket 3 ila zimepatikana nne utaenda kuangalia zipi zinakufaa ipi uiche , na maduka ya nguo ndio hatujapata duka moja na pia maduka ya simu umepata tatu bosi wangu nakuskiliza wewe." Dalali alizungumza bila kupumzika hio ndio sifa ya dalali lazima uwe na maneno mengi.
"Ooh okay sawa vyote ulivovitaja navitaka hivyo hivyo kisipungue kitu wala kisizidi kitu , hvyo vyote sina zina bidhaa ndani?"
"Ndio boss yani hapo wewe ni kwenda kubadilisha document tu na kuweka wafanyakazi unaowataka"
"Wambie hao mamiliki wawaache wafanyakazi kisha niambie ni kiasi gani kinahitajika kisha nikutane nao tubadilishane document kila mtu afe na chake" fahadi alizungumza.
"Sawa mkuu , ngoja niwasiliane nao kisha kila mmoja tukutane nao si hata leo?"
"Asaivi wasiliana nao me najiandaa hapa kisha utanambia wapi tunakutana"
"Sawa tajiri"
Kisha akakata simu , akatazama upande wa meseji alikuta zimetumwa kutoka kwa Maryam akazisoma kisha akaamua kumpigia iliita kwa muda kisha ikapokelewa.

"Haloo mke wangu"
"Mambo baby"
"Poa mzima wewe"
" me mzima , sijui wewe"
"Niko vizuri , sorry kwa kuchelewa kujibu ujumbe wako ulio ntumia asubuhi nilikua nimelala bado"
"Mhh unaamkaga saa ngapi na kazini unaenda saa ngapi au ndio mtoto wa mama"
"Hahaha me naamka muda wowote , alafu me ni king'asti wako nafanyaje kazi wakati mke wangu kazi unayo"
"Weeee koma me siweki mtu kibenteni, utafute kazi bwana maswala ya kukaa kutegemea mali za wazazi sio vizuri"
Maryamu angejua kua huyo mtu anapata hela kwa kuua watu angemkamata mara moja.
"Usijali utajua tu kazi yangu mke wangu me hua nafanya kazi nyumbani tu."
"Mhhh we haya tu , usije ukawa jambazi unaeibia watu ntakukamata mwenyewe "
"Hahaha hapana "
"Sawa basi vipi leo una ratiba gani jioni mume wangu."
"Aah hapana sina ratiba usiku ni hivi sasa naenda sehemu kufatilia vitu kisha nitakua free"
"Okey mume wangu leo nikitoka saa 10 njoo unipitie unipeleke home tupate dinner pamoja au unaonaje honey?"
"Wazo zuri kidogo leo nile mapishi yako"
"Hahaha me sijui kupika"
"Sawa tutakula chakula kibichi"
"Haya sawa mume wangu ntakupikia"
"Ok sawa wacha nijiandae basi nimalize mizunguko mapema niwahi kukufata boss wangu"
"Haya mume wangu , bye i love you and take care"
"Ok , love you too"
Akakata simu kisha akaenda kujiandaa kuelekea alipo dalali.

*******


Fahadi alifika kwa Dalali na moja kwa moja wakaenda sehemu ya kwanza kwa mzungu wakakabidhiana , akaenda kwa muhusika wa maduka ya nguo nae pia wakakabidhiana pia akaenda kwa muhusika wa maduka ya nguo nae pia wakakabidhiana hapo alikua hati miliki zotena pia alienda kubadilisha maswala ya TRA huko hakukua na usumbufu kutokana alikua na pesa kila kitu alimaliza siku hio hio na kukabidhiwa Document na leseni za biashara na kua mmiliki halali wa maduka ya simu maduka ya nguo pamoja na supermarket alikutana na wasimamizi na kuwapa utaratibu wa kazi anaoutaka yeye huku akiwaahidi kupandisha mishahara kwa wafanyakazi wake wote, kisha akamalizana na dalali ambae alimsaidia katika upatikanaji wa hizo bishara.

Mpaka anamaliza mambo yake ilikua imeshafika mida ya Maryam kutoka kazini, alipitia sehemu akanunua Maua mazuri yaliyokua kwenyw chupa yake kisha alifika posta maeneo ya Central na kuingiza gari ndani ila alikutana na ulinzi wa askari kama kawaida ya pale kabla hujaingia utakutana na maswali.
"Wapi unaelekea?" Lilikua swali kutoka kwa askari ambae anaonekana ni mpenda pombe maana alikua na tumbo kama mkoba wa kinyozi.
"Nimeitwa"
"Hilo ndio jibu la swali nililokuuliza au unataka ulale sero kijana?"
"Nimeitwa na inspector maryam"
"Unatakiwa unyooshe maerezo, kuna ishu gani ?"
"Si umuulize mwenyewe mzee me najuaje kaniitia nini "
"Kijana unajiona mjanja sio ngoja ipo siku tutakutana"
"Aah tushawazoea askar wa kibongo nifungulie geti, nikaweke wapi gari"
"Muulize Inspector maryam pakuliweka Gari"
Yule askari alimjibu nyodo Fahad, hakutaka kumjibu alitabasamu tu kisha geti lilifunguliwa na Fahad akaipaki gari sehemu ya maegesho akabeba Uwa lake zuri kisha akaingia nalo mpaka maeneo ya mapokezi akaulizia ilipo ofisi ya Inspector Maryam alielekezwa kisha akapiga hatua kuelekea ilipo hio ofisi.
Baada ya dakika moja alifika alibisha hodi akaruhusiwa kuingia na alimkuta inspector Maryam akiwa kwenye kiti akiwa ameinamia mafaili yake alipoinua uso wake alikutana na Fahad akiwa amesimama mbele yake.
Alitabasamu wakati anainuka kwenda kumkumbatia Fahad alijifanya anapiga saluti kama heshima na utani wa mapenzi .
"Hahaha unapiga saluti ya nini jamani waaaoooo mwaah mwaaah " alimkumbatia Fahad na kumshushia mabusu kadhaa
"Karibu mume wangu , yani umekuja mpaka ofisini jamani huogopi?"
"Niogope nini sasa Wife, wakati hii ni sehemu salama ambayo kila mwananchi hatakiwi kupaogopa"
"Ni kweli ila wengi wanapaogopa"
"Okay , zawadi yako hii" aliongea huku akimkabidhi mfuko uliokua na maua.

Maryam alipokea kisha akaufungua na kukutana na maua mazuri aliyabusu na kuiweka kwenye meza yake iliyojaa mafaili ya kesi mbalimbali.
"Wow maua mazuri yanananukia vizuri hata hivyo yamependezesha ofisi yangu"
"Usijali mke wangu ni jukumu langu kukupendezesha wewe na vitu vinavyokuzunguka."
"Thank you babby, karibu ukae ngoja nimalizie kusaini haya mafaili kadhaa kisha tuondoke"
"Okay saw"
Maryam alikabidhi kazi zake baada ya kumaliza kuzi saini kisha wakaondoka zao kuelekea nyumbani kwake.
Wakati wanatoka getini hawakumkuta yule askari ila wangemkuta fahad alikua ashapanga kumsemea kwa maryam.
Safari ilisonga mpaka kwenye supermarket moja walinunua mahitaji ya usiku ule kisha wakaelekea nyumbani. Waliingia ndani na kusalimiana na dada wa kazi.
"Amina , huyu ni mgeni wetu leo pia ni kaka ako unavyoniheshimu mimi dada ako basi na huyu muheshimu mara mbili yake maana yeye ndio Furaha yangu kila siku ulikua unaulizia lini utamuona shemeji ako basi ndio huyo" Maryam alitoa utambulisho.

"Jamaani kalibu shemeji , jiskie hulu " Amina aliongea na lafudhi yake ya kimakonde.

"Asante amina" Fahad alijibu
"Halafu nilikutumia meseji usipike "
"Ndio dada wala sikupika nilikua nakusubili wewe nikajua utakuja na yale madude sijui mapidha sijui pisha ah madude ya kizungu hatujui sie bwana."
"Hahaha hapana leo nitapika mimi, Fahad karibu ukae jamani umesimama kama mlinzi hapa kwako jiskie huru" Alimkaribisha akae Fahad maana muda wote alikua bado kasimama kwa sababu sio vizuri kama hujakaribishwa na mwenyeji wako ukae.
Maryam na Amina walielekea jikoni kwenda kupeleka mazaga waliyonunua.
"Dada, shemeji nzuli ajabu sijui nzungu au mwalabu mana mweupe yani aeleweki" amina akmuuliza maryam.
"Hahaha hapana bwana mpemba tu yule , andaa vitu ngoja nikajimwagie ntakuja kupika mwenyewe."
" sawa dada"
Maryama akatoka na kuelekea seblen .
"Baby me naenda kuoga basi nakuja"
Fahad wala hakutaka kumjibu akainuka na kumfata Maryam akambeba na kumbusu
"Aiii jamani amina atatuo..."
"Chumba chetu kiko wapi?"
"Kile pale cha mwisho upande wa kulia"
Fahad akapiga hatua na kuelekea chumbani , wakaingia ndani kisha akamshusha na kuanza kumvua yale mavazi ya kipolisi huku akimuimbia nyimbo ya Jay melody inayoitwa Nitasema , kama hujui mashairi ya hii nyimbo basi mapenzi huyajui .
Hayo yote yalikua mambo mageni kwa Inspector Maryam hakuwahi kufanyiwa wala kusikia mahala.

 

Usikose sehemu inayofuata🔥🔥 Kuna sehemu inayofata lipa shilling 1,000 tu nikuunganishe kwenye simulizo zangu zote zinazofata.


Digxam

FREE
VIEW