Maisha ya kimasikini husababisha watu kuingia kwenye makundi tofauti kwa ajili ya kupata riziki zao za kila siku, wapo wanaoingia kwenye makundi ya ukabaji, uchangudoa, uuzaji wa madawa ya kulevya, makundi ya wauwaji n.k ila hayo yote sio kila mmoja hua anapenda kufanya hivyo wapo ambao hawapendi ila ni msukumo tu wa maisha ndio huwapeleka kwenye makundi kama hayo.
Jina Langu naitwa Fatuma , naishi katika jiji La Daresalaam sehemu moja inayoitwa Buguruni , wengi wanaijua buguruni kwa sababu kuna sehemu inayoitwa Kimboka , hili eneo ni maarufu sana kwa sababu ukija hapa utakutana na kila aina ya wanawake haswa wale wa uswahilini waliokua wazuri na wasio kua wazuri basi ukija Buguruni Kimboka utawakuta wakiuza miili yao kwa bei rahisi tu.
Elimu yangu sio ya kuridhisha nilisoma mpaka kidato cha nne , ila sikufanikiwa kuendelea kutokana na hali ya familia yangu ilikua mbaya kutokana na baba hakua na kazi yenye kipato cha kukidhi mahitaji yote ya familia,pia mama alikua ni mtu wa nyumbani, kutokana na uhaba huo wa riziki ya baba kuna muda mwengine hua tunakula milo miwili mpaka mlo moja ila cha kumshukuru mungu hatukuwahi kulala na njaa.
Mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia ya Mzee Seif na Bi Warda kua wa kwanza na sikua na kazi ilikua ni jambo gumu sana hali iliyopelekea mimi kwenda kuanza kutafuta kazi sehemu tofauti tofauti ili kupata kipato cha kusaidia familia yangu japo kidogo.
Nilipitia maisha magumu sana katika utafutaji wa kazi nakumbuka sehemu ya kwanza kwenda kuomba kazi nilikutana na mambo ya ajabu sana,ilikua kiwanda kimoja cha rasta nilikwenda kwa jina sitokitaja.
Nilifika nikaelekezwa katika ofisi ya mtu anaeajiri wafanyakazi wapya, Niligonga mlango nikaruhusiwa kuingia ndani, nilimuona mbaba mtu mzima mwenye tumbo kubwa.
"Sh...shikamo" nilimsalimia huku nikiogopa maana alikua na sura ngumu kiasi.
"Unaniamkia unataka kuninyima nini bint" alinijibu huku akichukua box la biskuti lililokua juu ya meza kisha akachukua biskuti moja na kuila huku alikua ananitazama kwa jicho flani la kunitamani flani hivi ila akajifanya kama hana habari.
"Ah ...ah...hapana " nilimjibu huku nikionyesha uoga.
"Haya nakuskiliza" alinijib.
"Nimekuja kuomba kazi"
"Aliekuambia kuna kazi hapa nani?" Aliniuliza yule mbaba.
"Ha...ha..hapana sij..aambiwa na mtu nimekuja tu kuangalia nafasi za kazi"
"Kazi hakuna" alinijibu bila hata chembe ya huruma huku akiendelea kula biskuti zake, kiukweli nilikua nimeshikwa na njaa halafu zile biskuti nazitamani ila ndo hivyo yule mbaba mroho hata kunikaribisha jamani mh.
"Aya asante"Nilimjibu kisha nikaugeukia mlango ili safari ya kurudi nyumbani kwa miguu ianze.
Nilipogeuka ilikua kama kosa maana aliona umbo langu, hemu subiri kwanza kumbe nilisahau kuwambia kuhusu uzuri niliobarikiwa na mungu, nina pua ya kisomali , macho mazuri ya kulegea na kasura flani hivi kakipemba.Nilikua na ngozi flani hivi ya kipemba sio nyeusi wala sio nyeupe sana yaani ningekua na matunzo ningekua na ngozi nyeupe ila ndo hivyo dhiki za maisha zikanifanya rangi yangu ibadilike na kufifia. Mungu alinijaalia nywele za asili zilikosa kutiwa dawa kwa muda mrefu maana sikumbuki hata lini niliweka dawa ya nywele.
Tukija katika umbo langu utabaki hoi, kifuani chuchu saa 6 zilizoshiba , nikitembea na dela tupu ni kama nataka kutoboa kwa jinsi zilivyochongoka. Nina tumbo flati kiuno chembamba hips zilizotekeza pembeni vizuri na kushikamana na mapaja vema. Kwa nyuma nilifungasha mzigo haswa nikitembea wengi huona nafanya makusudi kwa jinsi ninavyoyachanganya maboga huko nyuma, wengine walikua wakidhani mimi nafanya michezo ya kwa mpalange ndo mana makalio yangu ni laini ila sio kweli ni uumbaji tu wa mungu ambao aliamua kuniumba, yaani kwa kifupi me mzuri ila tu sikua na matunzo kabisa. Turudi kwenye simulizi yetu.
Wakati nageuikia mlango ilikua ni kama kosa maana nilimuonyeshea ile shepu yangu vizuri alipagawa na kuinuka kisha akanifata maana nilikua nishaufikia mlango nilishangaa mkono wangu kushikwa nilishtuka.
"Unaenda wapi sasa binti" aliniuliza .
"Naenda nyumbani" nilimjibu.
"Kazi je hutaki"
"Si umesema kazi hakuna"
"Aaah jamani umbo hilo ukose kazi jamani" aliongea huku akinipapasa kiuno kusema kweli nilishtuka na kuutoa ule mkono wake.
"We mbaba vipi " nilimuuliza kwa uoga.
"Nipe penzi basi halafu kazi nakupa utakua haufanyi kazi ngumu nakuahidi mrembo"yule baba alinitongoza kavu kavu bila hata ya aibu , yani nimpe mwili wangu kwa ajili ya kupata kazi? Kujitunza kote tangu utotoni mpaka nafikia umri huu hakuna mwanaume aliefanikiwa kuugusa mwili wangu halafu huyu nimpe kiurahisi hivi hapana .
"Aka we mbaba me naogopa kama kazi hakuna mpaka nikupe mwili wangu hapana niache niondoke zangu" niliongea huku nikiutoa mkono wako ulioshika bega langu na kuanza kuondoka.
Nilifanikiwa kushika kile kitasa cha mlango ila sikufanikiwa kuufungua nilishikwa mkono wangu na kuvutwa kwa kazi nilikuja kufikia kifuani kwa yule baba akanibana mikono na kunilazimisha kuninyonya midomo yangu kiukweli nilikasirika sana maana ule ulikua ni ubakaji na kwa familia yangu ningeshuka thamani pia ningedhalilika.
Niliwaza cha kufanya nikajitahidi kutumia nguvu zangu zote kutoka mikononi mwa yule baba namshukuru mungu nilifanikiwa kutoka kwa yule mbaba pale pale teke kali nililrusha na kwenda kutua kwenye sehemu za siri za yule mbaba alipiga ukunga huo.
"Aaaaaaaah we mse**e malaya wewe unataka kuniua kizazi ku*ama*o "
Sikutaka kusubiri nikakimbilia mlangoni nikaufunga nikatoka kwenye ile ofisi na kuelekea mlango wa kutokea katika kile kiwanda.
Nilitembea kutoka katika kile kiwanda mpaka nyumbani , nilikutana na mama nilimsalimia juu juu na kuelekea chumbani kwangu hali hiyo ilimfanya apatwe na wasi wasi na kupelekea kuacha alichokua anakifanya na kuja chumbani kwangu.
Alinikuta nimekaa kitandani nimejiinamia akapiga hatua zake fupi fupi na kuja kukaa pembeni yangu na kunivuta upande wake kisha akanilaza mapajani mwake. Nilitulia huku nikiwa nimezama kwenye dimbwi la mawazo kiukweli kitendo alichotaka kunifanyia yule baba kilikua kikiniumiza akili yangu.
"Una shida gani mwanangu" aliniuliza mama ila nilikaa kimya zikapita sekunde kadhaa bila kutoa jibu lolote hali ilipelekea mama kuniuliza tena.
"Mwanangu kipenzi , niambie kuna shida gani huko ulipotoka"
"Mama nimeumia kwa kweli"niliongea huku nikionyesha hali ya majonzi.
"Kivipi mwanangu"
"Nilikuaga naenda kuomba kazi sehemu kufika kule naambiwa kazi hamna wakati nataka kuondoka yule mbaba ananivuta anataka kunibaka yani mpaka natoka pale ilikua mungu tu kanipa nguvu lakini leo ningebakwa mimi jamani mama" niliongea huku machozi yakinimwagika.
"Pole binti yangu , ni mambo ya kawaida kwa mwanamke katika utafutaji wake wa riziki , kikubwa kua na msimamo wako kama wanataka mwili wako kwa ajili ya kukupa kazi ni bora ukaacha kuliko kwenda kuishusha thamani yako mwanangu." Alinisi mama.
"Sawa mama nakuahidi hilo" nilimjibu mama.
Tuliendelea na stori zengine kisha nilienda kumsaidia mama kazi zengine pamoja na kuandaa chakula cha jioni.
Baba alisrudi jioni na kukuta chakula kimeshaandaliwa tukajumuika na mdogo wangu wa kiume ambae alikua darasa la tano. Baada ya kula tuliagana kila mmoja alilwemda chumbani kwake , cha kumshukuru mungu baba alipopata hela kipindi cha nyuma aliweza kuwekeza katika ardhi kisha akajenga nyumba kubwa tu ila haijamaliziwa kwa kupigwa rangi pamoja na vitu vyengine ila ni nyumba ambayo kila mtu anaweza kuishi ukizingatia sisi ndio ilikua ni kwetu haina budi kupapenda , nyumbani ni nyumbani tu.
Siku zilisonga huku nikiendelea kupata tabu katika utafutaji wangu wa riziki nilipata shida katika kuipata ajira au kibarua kuna sehemu nyengine napata utakuta kazi ngumu kuliko posho unayoipata, hali iliyopelekea kuacha kwenda kufanya kazi.
(
***********
Siku moja wakati natoka kuomba kazi sehemu moja. Wakati natembea barabarani nikiwa maeneo ya hospitali ya mkoa ya Amana, kuna gari aina ya Harrier Matako Ya Nyani ilipita pembeni yangu na kupaki kwa mbele yangu hatua kama 10 hivi. Nilipofika upande wa dirisha wa abiria niliona kioo kinashushwa kisha kuna Mama alikua amekaa upande wa dereva aliniita.
"Binti " ilikua ni sauti ya yule mama ikiniita niliangalia upande niliokuwepo sikuona mtu yoyote mwenye jinsia ya kike zaidi yangu na ya yule mama nikamheukia na kumuonyesha ishara ya kidole kua ni mimi anaeniita au kuna mwengine nae akajipu kwa kutingisha kichwa ishara ya kua ni mimi anaeniita nikaona sio mbaya huenda akawa ni mtu mgeni anataka kuelekezwa mahala.
Nilitembeza miguu yangu hadi kuifikia ile gari kisha nikamuinamia dirishani.
"Fungua mlango ingia ndani" alinambia yule mama.
Nikavuta kitasa cha mlango kisha nikaingia ndani ya gari yake.
Alikua ni mama flani wa kiarabu mweupe balaa alikua ameachia nywele zake ndefu nzuri na alikua ananukia ajabu kama jini jamani. Alinitazama vizuri kisha akavunja ukimya.
"Unaitwa nani binti" aliniuliza.
"Fatuma , naitwa Fatuma Mama" nilimjibu.
"Ooh jina zuri kama wewe yaani sijapata kuona binti mrembo kama wewe natamani ungekua mwanangu jomoni." Aliniambia yule mama.
"Asante" nilijibu.
Yule mama aliniangalia tena kama ananidadisi kisha akaniuliza tena.
"Unasoma?"
"Hapana"
"Unaishi wapi"
"Hapo mbele buguruni"
"Umetoka wapi"
"Nimetoka kuomba kazi sehemu ndio nilikua narudi hapa"
"Oooh ok sawa ,umepata kazi au"
"Hapana sijapata"
"Una ujuzi gani"
"Sina ujuzi ila kazi yoyote ninafanya kama ikiwa ina maslahi mazuri ."
"Oh ok sawa , umesema unaenda buguruni eeh"
"Ndio mama"
"Wacha nikupeleke , maana naelekea Tabata Barakuda" aliniambia.
Safari iliendelea huku akiniuliza maswali kadhaa kuhusu maisha yangu na mimi sikua na hiyana nikawa namjibu kwa usahihi kabisa mpaka tunafika maeneo ya Buguruni Sheli tulikua tushaongea mambo mengi mpaka kufikia hatua ya kuzoeana kama tuliokua tumejuana muda mrefu.
"Shika hii bussiness card yangu maana uliniambia huna simu , kesho utanicheki asubuhi ili kupanga ratiba ya kuonana na wewe ili nikupeleke kwenye sehemu ya kazi, pia chukua hii utafanya mambo yako madogomadogo" Aliniambia huku akinipa kadi yake yenye namba zake za simu kisha akanikabidhi na elfu thelathini , nilishtuka maana hatukua tunajuana akanisihi nichukue ikanibidi nichukue tu bila hiyana, nikaaga nae akaniruhusu na kumuahidi kesho nitamtafuta kwa wakati.
Nikashuka pale nikiwaza pesa niliyoipata leonikaiangalia ile kadi aliyonipa nikakuta imeandikwa MADAM WHITE inaonekana shuhuli zake ni maswala ya vipodozi na urembo mbali mbali niligundua hilo baada ya kusoma upande wa nyuma. JE NINI KITAENDELEA, SIMUIZI HII UTAIPATA KWA Tsh 3000