Mvua ilikua inanyesha na radi zilikua zinapiga pia upepo mkali ulikua unavuma kupigwa pigwa kwa kitu nilichokilalia kulinifanya nikurupuke nikaangalia mbele nikakuta ni maji ,nikataza na upande wa kulia pia maji nikamalizia na upande wa kushoto nako pia kulikua ni maji hapo ndio nikajua kua nipo baharini mkono wangu ulikua umefungwa na pingu kwenye chuma kimoja ambacho kwa kilikua kimekatika mahala ambako sikujua ilikuaje mpaka nikafungwa nacho. Nikaanza kutafakari pale nimefikaje na mbona nipo kwenye maji naelea nikapata akili ya kuangalia nyuma nikaona meli ikiwa imezama nusu kama ilivyozamaga meli ya TITANIC nikaona sasa huu ni wakati wangu wa kufa kwenye maji kwa bahati nzuri nilikua juu ya boti ambayo ilikua nayo imepinduka yaani chini kumekua juu na juu kumekua chini nikaangalia nyuma bado sikuona dalili ya mtu yoyote bali niliona baadhi ya miili ikiwa inaelea kwenye maji yale ya bahari .
Nikadumbukia kwenye maji nikaanza kugeuza kile kiboti kwa bahati nzuri nikafanikiwa japo ilikua kwa shida kwa sababu nafanya mambo mawili kwa wakati mmoja yaani huku nipo ndani ya maji natakiwa kuelea na huku nageuza boti, baada ya kuiweka sawa nikaanza kupanda nikaingia ndani ya ile boti nikatulia ili kuupumzisha mwili nikainuka juu kuangalia kama kuna msaada wowote ila sikuona jambo lolote zaidi ya kuiona ile meli inazama tena kwa mbali kidogo nikakaa kwenye kwenye kibenchi cha kwenye ile boti nikitafakari ilikuaje mpaka mimi nikafika pale na pia ni sababu ipi iliyofanya meli izame ?? Nikaangalia saa yangu nikaona ni saa 10:30 usiku huku mvua ikiendelea kunyesha nikaona nikizubaa hiki kiboti kitajaa maji nikaanza kuyatoa maji kwa kutumia mikono maana sikuwa na chombo cha kutole wakati naendelea kutoa yale maji nikaona ndoo inaelea ikabidi nijitose kwenye maji nikaifate nikaingia kwenye maji nikaitoa nikairusha kwenye kiboti changu nikapanda kwenye kiboti kile kisha nikaangalia kwa chini nikakuta makasia nikayachomoa na kuyafunga kwenye sehemu zake nikapata wazo la kurudi kwenye ile meli japo ilikua inaonekan kidogo maana meli huzama taratibu nikaanza kupiga makasia mpka maeneo Yale kwa bahati nzuri nikakuta kamba nikaichukua na kuifunga kwenye boti yangu kisha nikasogea mpaka pale kwenye chuma cha meli nikaifunga pia kisha nikajitosa ndani ya maji ili nikaangalie kama kutakua na kitu cha kunisaidia. bado nilikua na chuma mkononi kina kama urefu wa nchi 35 hivi ,nikasogea kwenye chumba cha captain nilikijua kwa sababu kuna picha za mtu mwenye vyeo na ni mzee mzee nilifungua friji ambalo lilikua upande upande nikatoa vyakula nikavirusha kwenye kiboti changu nikarusha na vinywaji nikafungua na kabati nikakuta over roll na mabuti nikavirusha ,kisha nikaona radio ya msaada (SOS) Pia nikaitia kwenye boti nikaangalia nikakuta bastola ya flashlight pamoja na pistol ndogo yenye magazine 2 . Kisha nikasogea kwenye chumba cha stoo nikakuta kimeingia maji mpaka yananigikia kiunoni nikaangalia kitu kinachonifaa nikaona mashine ya boti aina ya YAMAHA nikaibeba nikatoka nje nikalikata lile turubai futi 10 kisha nikalikunja nikaliweka vizuri . Nikarukia boti yangu nikaifungua ile kamba na kuifunga pembeni ya boti mambo yote hayo mkono wangu mmoja umefungwa na pingu na kwenye chuma nikaanza kupiga makasia ili kuondoka kwenye lile eneo ninacho shukuru mungu mvua na upepo vilipungua yalikua manyunyu na upepo wa kawaida , niliendelea kupiga makasia mpaka jua lilianza kuchomoza nilikua hoi maana sikupumzika hata kidogo . Asubuhi kama saa 1 na robo nilipumzika huku kiboti changu kikipelekwa na mawimbi taratibu,nikafungua mfuko uliokua na mikate nikatoa vipande vitatu vya mkate nikala pamoja na maji kidogo ,niliamua kubalansi chakula kwa sababu sijui nitakaa siku ngapi pale baharini na sijui lini nitafika wala lini nitaokolewa .
Vyote hivyo havikiniumiza kichwa ,vitu vilivyoniumiza kichwa ni kwa nini sikumbuki pia siwezi kuongea sauti haitoki kabisa.
Nilishangaa kila nikijaribu kuongea sauti inagoma, sikua na njia ikabidi niendelee na safari yangu nisiyojua ni wapi naelekea nilikua ni kama kipofu nisiyejua wapi naenda ile engine ya boti nilijaribu kuiwasha ila iligoma sikua na ujanja nikaicha mule mule nikawa natumia tu yale makasia.
Nilikaa kwenye bahari kwa siku nne bila kujua ni lini ntafika pwani pia ni lini nitaokolewa,chakula nilichokua nacho kilikua kimeisha na maji pia yalikua yameniishia nikaanza kutafakari ni vipi nitapona kwenye hili tatizo, siku nzima ilipita bila kutia kitu kinywani sikua na nguvu mpaka nikapitiwa na usingizi.
Nilikuja kushtuka kwa kusikia sauti za kunguru na ndege wale wa baharini, nikaamka kama mzuka kisha nikaanza kuangaza kwenye kila kona ya dunia kwa mbali nikaona kama kisiwa nikachukua makasia yangu nikaanza kukifata kisiwa nilijithidi kwa kadri ninavyoweza ili nifike kwenye kile kisiwa maana njaa pamoja na kiu vilikua vinanisumbua mpaka vilinifanya nipungukiwe na nguvu kwa kiasi fulani.
Nikafika mpaka kwenye kile kisiwa kilikua kikubwa na kina milima mikubwa na kisiwa kimesheheni uoto wa asili miti imejaa kila kona .
Nikashuka nikaanza kukivuta kiboti changu mpaka nchi kavu nikafunga kamba kwenye gogo ili hata maji yakijaa kile kiboti kisiondoke. Nikachukua pistol nikaiweka nyuma japo sijui kuitumia ila nitajua mbele ya safari. Muda huo bado lile chuma ambalo nililokua nimefungwa nalo bado lilikua mkononi.
Nikatoka kwa mwendo wa uangalifu nikasogea mpaka kwenye mwanzo wa ule msitu nikakutana na kitu cha kutisha , ilikua na mwili wa binadamu ambao umeoza ukiwa umefungwa kwenye mti inaonekana ile maiti haina siku nyingi kama sio siku 3 au 4. Moyo ulijawa na hofu maana ni mara yangu ya kwanza kuona kitu kama kile.
Sasa nafsi zikawa zinavutana moja inaniambia niingie nyengine inakataa ,ila moja ikashinda kwa sababu nilikua na njaa nikaanza kuingia kwenye ule msitu kwa uangalifu zaidi maana nimeshaanza kukutana na vitu vya ajabu nikalishika chuma langu liwe kama silaha nikaanza kunyata kama mwizi nilisogea mbele nikakutana na mti ambao unatoa kitu kama utomvu ila ni mweusi una mfano kama wa mafuta nikayagusa yalikua malaini nikaona hii ndo njia ya kutoa ile pingu , nikapaka kwenye mkono wangu cha kushukuru mungu nilikua nimekonda kidogo kwa hio ikawa rahisi kwangu mkono kupita nikafanikiwa kuutoa mkono kwenye ile pingu ambayo ilikua imejifunga kwenye chuma nilishukuru mungu.
Nikaendelea na safari huku nikiokota matunda ambayo sijui yana sumu au hayana ila nilichokifahamu mimi ni kula tuu , njiani nilikutana na kimto cha maji safii nikachuchumaa nikaanza kunywa maji ili kulipoza koo .
Baada kumaliza kunywa maji nikaokota baadhi ya matunda na kurudi nilipotoka ,nikafika kwenye kiboti changu nikaingiza matunda yale na mimi nikaingia ndan ya boti nikianza kutafakari maisha haya mapya ya kisiwani .
Nilikaa mpaka jua likazama hali ilikua bado imetulia ila kwa mbali niliskia kitu kama tarumbeta au vuvuzela linapigwa lilipulizwa kwa mara tatu ,POOOOOOOOONHH!!! POOOOOOOOONHH!!! POOOOOOOOOOOOOONH!!!!!!!!!!
Nilianza kuingiwa na hofu na uoga wa hali ya juu nilijikunyata kama kitoto cha kuku. Nikaanza kusikia ngoma kwa mbalii nikainuka na nikaanza kuangaza maeneo ya kwenye kisiwa kwa mbali juu ya mlima nikaona kama mnara umewashwa moto yaani unaungua ila mda ule wa mchana sikuuona ikabidi nitulie tuu. Nilikaa kwenye kiboti changu huku baridi likinipiga mpaka nikapitiwa na usingizi.
_____________★__________
Asbuhi niliamka nikiwa na nguvu tele nikajirusha kwenye maji nikaanza kuogelea kwa dakika mbili ili kuuchangamsha mwili kisha nikarudi ndani ya boti nikavaa nguo zangu nikachukua na bastola pamoja na lile chuma ambalo nimelifanya kam rungu kwangu.
Nikaondoka mpaka ufukweni nikakaa kwenye kigogo nikianza kutafakari " hiki kisiwa kinaonekana kizito pia kina mambo ya kutisha je nitaweza kuwa hai , NITAWEZA TUU, lakini sijui ni vipi nitaweza kujikomboa kweli?? Pia mbona nikijaribu kutoa sauti haitoki kwa nini??na ilikuaje mpaka nikiwa kwenye ile ajali na ilisababishwa na nini ??? Mh ok haina jinsi ila ngoja kwanza nijifundishe hii bastola ili hata likitokea la kutokea huko porini nijue kujiokoa " Niliwaza.
Nikaitoa bastola ile nikajarib kupiga ikakataa, nikajaribu tena pia ikagoma nikagusa juu nikaona kinasogea nikaikoki kisha nikabonyeza trigger ukatoka mlio mkubwa PAAAAAHHH!!!! nilifurahi kwa kufanikiwa nikapiga tena nikamalizia kwa mara ya mwisho kisha nikairudisha sehemu niliyoiweka mwanzo.
Nikaingia msituni mule kwa mwendo wa tahadhari nikasonga katikati ya msitu nilikuatana na nyoka wengi lakini nilikua nao makini japo nilikua na uoga.
Kwa mbali nilianza kusikia michakacho kama ya watu wakikimbia kuja nilipo mimi nikajibanza kwenye mti baada ile michakacho kukaribia nilipo mimi ikatulia nahisi walikua wamejua kua kuna ugeni nilikua sifahamu kama ni watu au ni mnyama. Ikanibidi nianze kutoka kwenye mti ili nione ni kitu gani. Wakati nasogea tu niliskia sauti ya kitu kikija kwa kasi ikanibidi nigeuze kichwa kikapita kwenye ngozi yangu ya shavu Fyuuuuh!! Nikahisi maumivu kwa kiasi flani hivi nikagusa shavu nikaona linatoka damu hapo ndo nikajua nipo kwenye hatari ikanibidi nianze kukimbia nilitoka kwa kasi ya ajabu nilikimbia lakini niliona ni kama watu nyuma yangu wananikimbiza lakini ni weusi balaaa wakaanza kunirushia mishale pamoja na mikuki lakini niliikwepa kuna mmoja wao nikamsikia anatoa yowe la nguvu kisha wakasimama ila mimi sikutaka kusimama nilizidi kukimbia ila kwa mbele nikakuta kipande cha mtu kimesimama halafu kashika Rungu kubwa na mimi nikashika chuma langu nikakimbia kwa kasi mpaka alipo yule mtu nikalirusha ila akalikwepa na yeye akanirushia rungu la lake likanipata la tumbo likanifanya nidondoke mpaka chini niliugulia kwa maumivu ila nikapata ujasiri wa kuinuka tena sikujali kama lile jitu au ni mzimu maana alikua anatisha sana nikaanza kumfata tena kabla sijamfikia nilihisi kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni nikakiangalia ni kama kijiti cha kuchokolea meno nikaongeza hatua mbili mbele nikadondoka kama mzigo na kupoteza fahamu palepale.
★★★★★★★
Nilikua nahisi kama nachezewa pua yangu ikabidi nishtuke kutoka kwenye usingizi mzito nikaona vijitu vidogo vidogo vinavuta pua yangu halafu vinacheka cheka nikaangaza nikajiona nimefungwa na kamba kichwa chini miguu juu na mikono pia imefungwa pia.
Vile vijitu vinaonekana ni vitoto ila vilikua pia vinatisha sana nikaangalia mazingira ya pale nikaona watu wakiwa kwenye shuhuli zao kina mama walikua wanarangi nyekundu na kina baba wanarangi nyeusi nikafahamu hii ni tamaduni yao ila nitatokaje kwenye huu msala na wanaonekana hawa ni wala watu kwa mbele niliona ule mnara ambao jana ulikua unawaka moto nikaona bora nisubiri mda wangu wa kufa ufike tuu nife maana siwezi kutoka kwenye mikono ya hawa majamaa.
Masaa yalikatika kiza kikaingia mara nikamuona jamaa anapita na pembe la tembo akaenda hadi kwenye ule mnara akapanda mpaka juu halafu akaanza kulipuliza mara tatu kama nilivyokua nasikia jana usiku. Baada ya mda nikaanza kusikia michakacho na sauti za wanyama, wakaja majamaa wawili ikafungua nakwenda kunifunga kwenye mnara pale chini kisha wakaanza kuvuta kamba na mimi nikaanza kuinuliwa mpaka juu nikawa naning'inia ila mara hii kichwa kipo juu miguu chini nikaanza kuomba mungu aniokoe na hili janga ngoma zikaanza kupigwa kuna mtu akaja na moto anataka auwashe ghafla kamba ikakatika nikaanza kudondoka kuelekea chini ila nikashukuru mungu nilitua vizuri ila mguu uliteguka kufumba na kufumbua akatokea mtu alievalia kininja akarusha kitu kama kifuuu kikaanza kutoa moshi wa ajabu ambao ulisambaa kote pale nakufanya watu wasionane akaja akaninyanyua na kuanza kukimbia japo sikua na hali nzuri ila ilinibidi kujikaza tukakimbia kwa umbali mrefu mwili ulikua umechoka ila nilizidi kujikaza.
Baada ya kutembea kwa dakika kama 50 ndipo tukafika mahala
"Wait!! (Subiri) "
Kwa mara ya kwanza jamaa alizungumza maana safari yote tulikua kimya ila pia kilichonishangaza ni sauti ya kike ambayo ilitoka kwa yule mtu nilishindwa kumtambua kwa sababu alivaa ninja, nikataka kumjibu lakini sauti haikutoka nikabaki pale pale aliponiambia nisubiri,
Akasogea mpaka sehemu yenye majani makavu akasafisha safisha akaondoa majani kukaonekana kama kunanjia ambayo inaelekea chini akafungua mlango akainama kidogo akatoa jiti ambalo kwa juu limezungushwa tambara kisha akaliwasha moto kidogo tukapata mwanga.
"Let's go (tuondoke) !!"
Nikamfuata mpaka pale alipo akanza kuingia chini na mimi nikamfata,
"Close that door(funga ule mlango)"
Nikarudi juu nikaufunga kisha nikashuka chini japo kulikua na taa bado giza lilikuwepo tukatembea chini kule mpaka kwenye eneo moja kubwa ambalo liko kama chumba ila kuna makorokoro mengi ,
"Sit here(kaa hapa)"
Nikasogea mpana sehemu aliyonielekeza nikae.
Akaelekea pembeni kwenye meza sijui alikua anatafuta nini kisha akaanza kuvua gloves zake ,akavua na viatu akatoa na pistol akaiweka juu ya meza kisha akavua Ninja lake kwa nyuma alionekana mzuri alikua ana nywele fupi alikua na shepu flani ya kuvutia japo si kubwa sana maeneo ya shingoni alikua na mchoro ila sikuuona vizuri kwa sababu nilikua mbali .
Alipogeuka!!! nilishangaa alikua ni msichana mzuri mwenye pua ya kisomali midomo membamba halafu pia ana chuchu konzi a.k.a saa 6 ila ana asili ya kizungu , aliponiona namuangalia sana Akatabasamu!! Kisha akaja nilipo mimi kwa hatua za taratibu mpaka nilipokaa mimi akanitazama kwa sekunde chache kisha akaenda kwenye ile meza aliyosimama mwanzo akachukua chupa ambayo ndani ina maji akaniletea nikaipokea huku nikimtazama usoni nikanywa yale maji taratibu kisha nikaweka pembeni ile chupa.
"What is your name??(jina lako nani)"aliuliza
"You can't talk??(huwezi kuongea)"
"Am asking you, what is your name and where are you from???(nakuuliza ww, jina lako ni nan na unatokea wapi)". Aliongea kwa hasira baada ya kuona mimi simjibu maswali anayo niuliza.
"Son of bitch( mtoto wa kahaba)"
"You are dumb of deef (wewe ni bubu au kiziw)??"
Nikatikisa kichwa akakaa kwa sekunde kadhaa kisha akaja na peni na daftari.
"Write here ,your name and where you came from also why are you here(andika hapa ,jina lako na ulipotoka na kwa nini upo hapa)"
Nikachukua daftari na ile peni kisha nikaandika
"SILIJUI JINA LANGU ,PIA SIJUI NILIPO TOKA HALAFU SINA KUMBUKUMBU ,KITU KINACHONIPA SHIDA NI SAUTI YANGU HAITOKI ILA NAWEZA KUONGEA"
Nikampa ile karatasi akaisoma kisha akaniangalia kwa makini akasema
"Usijali baba yangu alinifundisha vitu vingi kwenye haya maisha ,kuna baadhi ya miti nitakupa itakusaidia matatizo yako hayo uliyonayo "
Nikamuonyesha alama ya kushukuru
"Ok sawa,utalala hapo kesho asubuhi tutajua nini cha kufanya, usiku mwema"
Akaniaga kisha yeye akaelekea sehemu yake ya kupumzika akajilaza ,mimi nikakaa pale nilipoambiwa ndio sehemu yangu ya kupumzika taratibu kutokana na misukosuko niliyoipata leo mwili ulichoka ghafla nikaanza kujinyoosha nikapitiwa na usingizi Fofofo!!!
★★
Taratibu nilianza kufungua mboni za macho yangu nikaangaza alipokua amelala yule msichana lakini sikumuona nikainuka zangu taratibu nikaelekea pale kwenye ile meza nikakuta kuna picha nikaichukua na kuitazama kwa ukaribu nilimuona yule msichana yupo na mtu mzima nikazitazama ile picha ila nilishtushwa na sauti ya yule mwanamke
"Waoow umeamka ,unaendeleaje"
Nikageuka kisha nikatabasamu nikatingisha kichwa ishara ya kua niko sawa
"Oooh sorry nilisahau kumbe huwezi kuongea , ok nimekuja na dawa hizi ninaimani zitarudisha sauti yako itakua kama kawaida ngoja niziandaea"
Alikua amekuja na popo watatu pamoja na miti miti kwanza akachukua jiwe akaanza kuisugua ile miti halafu akanichemshia baada ya dakika kama ishirini akatoa na kunipimia kwenye kikombe
"Hii dawa ni nzuri itarudisha kumbukumbu zako poa itarudisha sauti yako ila kua na imani nayo itafanya kazi bila wasi wasi"
Akanipatia kikombe nikaanza kunywa nilimaliza vikombe vitatu japo ilikua ya uchungu ila sikuwa na njia nyengine ghafla nikapoteza fahamu .KAMA UNAHITAJI MUENDELEZO WAKE UTAIPATA KWA TSH 3000 UNAWEZA UKAWASILIANA NAMI KWA NAMBA 0657192690 WHATSAPP... 0629169248 KAWAIDA.