Notifications
Clear all

FAHAMU JINSI YA KUTENGENEZA HESABU ZA BIASHARA ILI KUPATA FAIDA

1 Posts
1 Users
0 Reactions
1 Views
(@technically)
Posts: 3
Balance 0.000
Topic starter
 

Njoo tujadiliane kupitia thread hii

Moja kati ya hesabu za biashara ni taarifa ya mapato na matumizi. Hii taarifa ni muhimu sana kwa sababu ndiyo ina onesha kama biashara imepata faida au hasara
Kwenye video hii nitaeleza jinsi ya kutengeneza taarifa ya mapato na matumizi ili uweze kufahamu kama biashara imepata faida au hasara
TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI
Taarifa ya mapato na matumizi imegawanywa katika sehemu zifuatazo:
* Taarifa ya mauzo ya bidhaa au huduma
* Taarifa ya gharama za kufanya mauzo
* Taarifa ya gharama za uendeshaji wa biashara
* Taarifa ya gharama za kifedha na uchakavu wa vifaa
* Upatikanaji wa faida au hasara
AINA MBILI ZA FAIDA YA BIASHARA
Katika utengenezaji wa taarifa ya mapato na matumizi, taarifa ina onesha aina mbili za faida ambazo ni
(a) Gross Profit
(b) Net Profit
o GROSS PROFIT (FAIDA KUBWA)
Faida kubwa hupatikana kwa kuangalia uwiano baina ya mauzo ya bidhaa na gharama za kufanya mauzo
o NET PROFIT (FAIDA HALISI)
Faida halisi hupatikana kwa kuangalia uwiano baina ya mauzo na gharama zote zilizofanyika katika biashara

Kama wewe ni nfanya biashara unahitaji huduma hii njoo kwenye comments section tuelimishane.

 

Gross

 
Posted : September 18, 2025 6:33 am