Niko Oman 🇴🇲 kuna simu nyingi sana mbovu na mzima zinauzwa bei rahisi sana.Watu mliopo bongo mkitumia vizuri hii platform tutafanya kazi,achana na mambo ya kizamani eti tuma mzigo nikutumie pesa au leta mzigo nikupe pesa ukisha beba mzigo ukifika story ubadilika nakuambiwa makubaliano mapya tuuweke hapa Officini mteja akipatika nitakujulisha au mtu mwingine anabadilika utafikiri sio yule alikuwa akuwashawi ubebe mzigo,nimeishapoteza sana hela kwasabu siwezi kuwa na muda wakukaa dukani kwako kila siku.
Hii tabia watu wengi wanayo huko bongo watu wanapenda sana zuluma,hizi platform kama hizi naamini kunawatu wanazichukia kwasabu huko mbeleni kila mtu atakula kulinganana na urefu wa kamba yake.
Kuna jamaa moja pale Duse alinipiga computer mzigo mzima wenye thamani ya 2m toko Kamipiga siamimi mtu hapa bongo.
Niko Tayari kutumia hii platform inafanya kila upande kuwajibika na kufanya biashara za uwazi na ukweli.
@rebecca Bongo biashara nyingi ziwe za online au Dukani zimeja utata,juzi niliuziwa TV fake nikarudi nikabailishiwa nikapewa tena fake nikachoka nimeamua kutulia.
Kutoka ni kazi sana kwasabu ya mazingira.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣