Chama cha upinzani Tanzania Chadema kinatarajia kuchagua mwenyekiti wake Januari 21. Mpaka sasa Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi hiyo, ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe, ambae anatetea kiti chake.
Maandalizi ya kuelekea uchaguzi huo, tayari yameibua gumzo kubwa huku baadhi wakihisi kuwa matokeo ya uchaguzi huo yanaweza kuleta mpasuko mkubwa katika chama.
Tupe maoni yako kwakuchagua mgombea moja wapo na kumpigia kura hapo chini.
@admim asante!
@Mshangazi Huyu baba anaenda kwa Rais wa Tanzania.Ebu sikiliza hii https://www.youtube.com/watch?v=t2HTUg9LTMw
@veronica-victor Tundu sio mtu wakushindananae atakuaibisha vibaya mno.
@Uhai Marko 10:25 ni rahisi Ngamia kupenya katika tundu la Sindano,kuliko Mwamba kumshinda Lissu.
@veronica-victor Mwamba angekubali ushauri wa family yake mambo yasingekuwa mengi hivyo.Uongozi unaokuja vyama vyote wajipange,inakuja safu ya wakata umeme,vyama vyote wajipange upya mchakamchaka unakuja sio wa kitoto. Kesho mapema na chukua card ya Chadema pia natoka 100k kama mchango wangu na Imani yangu kwa Tundu: 1.Lissu 2.Heche 3.Lema
@veronica-victor Mimi ni mwana ccm lakini Lissu akitangazwa Mwenyekiti Chadema nahama ccm 🙅♂️🙅♂️🙅♂️🙅♂️🙅♂️🙅♂️
@veronica-victor Leo mkimtangaza Tundu Chadema nawachangia 100,000.
@Neema mimi 20,000 yao ipo wakifanya kweli naomba control number hizo pesa tunamtumia Lisu moja kwa moja.
Wapenda Amani tuko CCM endelea kupambana na hali zetu.
Wote matapeli wa kisiasa.
Tundu Lissu amechukua usukani wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema.
Lissu amemng'oa madarakani Freeman Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kama mwenyekiti kwa miongo miwili.
Mbowe amekuwa wa kwanza kukiri kushindwa na kumpongeza Lissu kupitia mtandao wa X.
Timu ya kampeni ya Lissu pia imetumia mtandao wa X kutangaza ushindi wake.
Matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne usiku yanaonesha kuwa Lissu amepata 51.5% ya kura zote dhidi ya 48.3% alizozipata Mbowe.
Mara baada ya wagombea wakuu Mbowe na timu ya kampeni ya Lissu kutuma salamu za matokeo kupitia mtandao wa X, wakala wa Lissu kwenye uchaguzi huo na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema aliwaambia waandishi wa Habari kuwa Chadema ndiyo imeshinda.
"Chama kimeonesha demokrasia iliyokomaa… huu ulikuwa uchaguzi huru n awa haki kabisa, na umerushwa mubashara na vyombo vya habari. Watu wote wameliona hilo," amesema Lema.
Ilikua ni ngumu Mwamba kutoboa kwenye huu uchaguzi.
Hongera Mh Tundu Lissu.
Pongezi Mh Tundu Lissu.
Pia pongezi kwa John Heche.
Kapitwa parefu.
Hii inatwa Demokrasia.