#Mabadiliko.
Mabadiliko tunayoenda kuyafanya kama ifutavyo.
#Visitors Members
Itakulazimu ku login au kujisajili kuingia kwenye Forums zote,tutaacha baadhi zitakazoonekana kwa visitors wetu.
#Registered Members.
Kuna baadhi ya contents ,Forums au Categories utaweza kuingia lakini itakulazimu kulipia au kuwa na Trade Bond au Pay Trade ili kushiriki au kununua,nfano kama,minada na baadhi ya majukwaa ya kuuza na kununua.
#Registered Members
Registered Members wenye accounts za kulipia za Pay Trade na Trade Bond zenye dhamani ndogo pia kuna baadhi ya majukwaa wataweza kuingia lakini itakuwa ngumu kushiriki kama ku comments au Kubid bidhaa na kuuza au kununua.Lengo la madaliko haya ni kuboresha huduma na kuondoa changamoto mbalimbali ikipo
#Registered Members wenye Trade Bond na Pay Trade.
Utatumia Trade Bond au Pay Trade kama dhamana ya kununua bidhaa kwenye Platform zote online .
Ukifanya Binding bila kuwa serious na bidhaa Bond yako itatumika pia kumlipa muuzaji.
Nawatakiwa heli ya mwaka mpya 2026 watumiaji na wapenzi wote wa Digxam
Share hii post kisha subscribe kupata update kwa comments.
Pia tunakaribisha maoni na ushauri juu ya uamuzi huu,kila mdau atoe maoni yake.
by Digxam Team.
Haya mabadiliko yatatumiiza sana!
Nfano mimi nauza simu zangu kupitia kwenye planform ya simu wateja wangu wanalipa pesa kupitia kwa admin kisha namtumia mteja wangu simu baada ya kupokea simu mteja ana mtag admin kwamba kapata mzigo wake biashara imeenda vizuri Admin anaitumia changu je uoni kama nitashindwa kuingia kwenye forum ya simu nakukosa wateja kabisa?
Kwakifupi watu wa chini tunaumia kila sehemu ndio kwanza wateja wameanza kuzoe hii mifumo yenu kwanini msingoje kidogo kwanza angalau tufanya biashara ili tulipe Trade Bond kilakitu kiende sawa?
@fundi-simu Asante kwa maoni yako,
1.Trade sio lazima deposit cash kwenye account zetu,unaweza pia kupata Trade bond kwa kuweka dhamana ya kitu chochote kwetu officen.
2.Trade Bond unaweza kupata kwaku dhaminiwa na mtu mwenye ajira ya kudumu.
3.Unaweza kuwekewa dhamana na mtu mwenye Duka.nk
jaribu njia hizo tatu mkuu,haya mabadiliko tunataka kuyafanya sio kwa ubaya bali tunakuwekea mazingira mazuri ya biashara ya online kwa baadae.
@moderator Kaka hizo njia ni politics tupu nilishafatilia gharma za kupa Trade bila deposit ni ngumu sana nikubwa kuliko kuweka depost cash kwenye account.
Chonde chonde mkuu niko chini ya miigu yako.
Niko pamoja nanyie kwenye upande seriousness kwenye biashara kila mtu ashinde mechi zake madiliko ni muhimu sana.Mimi natumia app yenu kwasabu ya usalama kwaiyo kiongeza mbinu za kubana watu wenye mawazo potofu wakiamini online ni sehemu ya kunfa mizaa sio kweli.
Concern yangu kwenu iko hivi mimi ni subscribe nachangia 1,000 kwa mwezi kuwezesha huduma hii iwepo kwanini watu kama sisi tusipewe angalau kipaumbele tuka pass kwenye moderation system naumia sana kutuma ujumbe kisha nikaambiwa waiting for moderator au approve hili buku nachangia la nini?
@zaitun Asante kwa maoni na ushauri
jambo hili tunalifanyia kazi wakubwa zangu nimewatag tungoje watupa mrejesho.
Asante sana kwa kuchangua Digxam
Wabongo ni wageni wa touchingly kunasiku nikuwa naongea na rafiki yangu nje ya online nikamwambia huu ujinga wataukomesha soon tena last week kama nilikuwepo lazima ifike muda tuwe serious kama maisha yalivyo.
Online software kama hizi utakovyo kuja ndivyo utapokelewa watu wanajifanya kuzoze techinalojia nakufanya sandakalawe kisa mtu ana bando kala ndondo na ugali kashiba sasa wale mlinifanyia fujo kwenye post yangu ya biashara zangu njoo huku mtoe milio kuanzi 2026 hakuna kuingia kwenye biashara za mtu na kumuleta uzushi mala bei gani mala nimepanda dau bila kuwa na uwezo wa kununua @kabanza
Hii ilikuwa weakness kubwa sana kwenye mifumo yenu baada ya last year kuzindua hii future ya Trade Bond nfumo uliowafukuza wahuni wote nakukimbilia kusikojulika sasa zamu ya wazushi twende mdogo ndogo tutafika mazee.
Hii itaongeza idada kubwa ya watu kuendele kutumia huduma zenu nikipo mimi mpenda amani mtoto wa chuga ,big up sana.
Mko sawa kabisa.
Kila Tarehe 27 Mwisho wa mwezi,tunapakia Container kutoka Japan kwenda Dar✅ Lipia mzigo wako mapema week moja kabla ya mzigo kuondo.✅✅👍💪🙏🏿
Mbona mumekata umeme mapema kabla ya muda?