Notifications
Clear all

Dawa za kuondoa harufu mdomoni

1
Topic starter

Mtu ambae anajua dawa ya kumaliza tatizo la kunuka mdomo nisaidieni!

Napiga mswaki mara tatu kwa siku, nimetumia mouth wash mpaka nimechoka, nimetolewa tonsils lakini wapi!😔😔

Nisaidie jamani nahisi kwenda maporini nikaishi na miti na wanyama, sababu nimeachana na mpenzi kisa tatizo hili, darasani nilifanya vibaya kisa tatizo hili. Nimetumia gharama kubwa kununua madawa wapi.😭

Mtu aliyewahi kuwa na tatizo hili na akapona aniambie basi na mimi niishi kama binadamu wengine.

Nipo Dar, nahitaji msaada wenu !

1

Pole sana.

  • Tatizo hili huweza kumkumba mtu wa jinsia yoyote na anaweza akajijua au asijijue kama mdomo wake unatoa harufu mbaya.

Tatizo la harufu mbaya mdomoni husababishwa na mambo mbalimbali, ila sababu kubwa ni maambukizi ya bakteria au protozoa na kuoza kwa mabaki ya chakula.

 

Tatizo hili huweza kumkumba mtu wa jinsia yoyote na anaweza akajijua au asijijue kama mdomo wake unatoa harufu mbaya.

Binadamu sote tuna bakteria wa asili kabisa ambao kwa kawaida hawana madhara mdomoni kwetu na husaidia kumeng’enya mabaki ya vyakula pamoja na kupambana na vijidudu vya magonjwa.

Hawa ni bakteria wazuri kwetu na tunatakiwa kuwatunza kwa kutotumia vibaya kemikali kali na dawa ambazo zinaweza kuwaua, maana wakifa tutashambuliwa na bakteria wanaosababisha magonjwa kwa urahisi zaidi.

Kuna mambo mengi ambayo yanachangia mdomo kutoa harufu mbaya, miongoni mwa hayo ni pamoja na uchafu wa mdomo, magonjwa ya kinywa na meno, maambukizi katika njia ya hewa, kuoza kwa mabaki ya chakula mdomoni ambayo hubaki tusipopiga mswaki, uvutaji wa sigara, mdomo kuwa mkavu kwa muda mrefu, matatizo ya sukari, ini na figo.

Bakteria huozesha mabaki ya chakula ambacho hubaki kama mtu hatopiga mswaki. Pia bakteria hawa huweza kuongezeka na kurundikana katikati ya meno, kwenye fizi na kwenye ulimi na kuendelea na taratibu zao za maisha ikiwa ni pamoja na kutoa takamwili zao ambazo huongeza harufu mbaya mdomoni. Wanaweza pia kuua seli za mwili na kuzifanya zikaoza, uozo huo pia huongeza harufu mbaya mdomoni.

Tatizo hili huweza kutokea kwa sababu ya uwapo wa bakteria wanaosababisha harufu mbaya kwenye eneo la ndani zaidi ambako mswaki haufiki. Matokeo yake ni kwamba, hata ukipiga mswaki, wanaendelea kuwapo na harufu inaendelea.

Kwa tatizo hili, pata ushauri wa daktari na tumia dawa zote vizuri kabisa kama utakavyoelekezwa

 

Tushukuru kwamba kuna dawa nyingi na za bei nafuu kutibu tatizo hili na linatibika kabisa. Cha kwanza kabla ya yote katika matibabu ya tatizo hili ni kujua chanzo cha tatizo.

Muda mwingine unaweza kujitathmini mwenyewe, muda mwingine unaweza kusaidiwa na daktari. Anza kwa kupata ushauri wa daktari, hususan daktari wa kinywa na meno.

Ukijua chanzo cha tatizo hili matibabu yake ni rahisi zaidi.

Ikiwa umepatwa na tatizo hili, unaweza ukatumia dawa za kusukutua kama Hydrogen Peroxide, Chlorhexidine, Povidone-Iodine, Listerine. Hizi husaidia kusafisha mdomo vizuri na kwa urahisi zaidi, kuua bakteria mdomoni na kuleta harufu nzuri.

Dawa za meno husaidia kuondoa mabaki ya chakula, kupunguza vijidudu mdomoni na kuondoa harufu mbaya. Mfano ni Colgate, Whitedent na Sensodyne.

Dawa za kuua bakteria (Antibayotiksi),

Hizi ni dawa mahsusi kabisa kwa ajili ya kuua bakteria na kutibu magonjwa au maambukizi wanayoyasababisha.

Utashauriwa na daktari kulingana na aina ya wadudu ambao unao.

Pata ushauri wa daktari kisha tumia dawa hizi vizuri kama utakavyoelekezwa

Mambo ya kuzingatia, tatizo la harufu mbaya hutibika kwa urahisi na gharama nafuu, anza kwa kuhakikisha usafi wa mara kwa mara wa kinywa na meno.

Piga mswaki na/au sukutua kwa kutumia dawa ya kusukutua kila baada ya mlo na mara tu baada ya kuamka.

Endapo hata ukipiga mswaki na kusukutua bado harufu mbaya inaendelea, basi pata ushauri na matibabu kutoka kwa daktari wa kinywa na meno.

Tumia dawa zote vizuri kama utakavyoelekezwa na madaktari na wataalamu wa dawa .

 

Leta Tangazo lako la Biashara Tukutangazie kwa Gharama na fuu sana.wasiliana nasi:advertise@digxam.site au Whatspp +8180 2071 7421 or click here.

0

Nikutumie dawa za kinyeji utaweza kuzitumia?

0

Umeenda Hospital?

0

Mkuu mimi sio doctor ila nakupa first aid tumia dawa ya meno ya colget inaitwa max fresh.

0

Harufu mbaya ya mdomo inayosababishwa na mate ya koo inaweza kuwa ni ishara ya shida ya kiafya, kama vile kuvimba kwa koo au koo la tumbo. Ni muhimu kumuona daktari wako ili kugundua chanzo cha tatizo na kupata matibabu sahihi.

Kwa kuongeza, unaweza kuchukua hatua zifuatazo ili kupunguza harufu mbaya ya mdomo:

1. Kunywa maji mengi - kunywa maji mengi husaidia kuondoa mate ya koo na kusaidia kudumisha unyevu kinywani.

2. Safisha meno yako mara kwa mara - safisha meno yako mara kwa mara na kwa uangalifu. Piga mswaki mara mbili kwa siku na kutumia dawa ya kusafisha mdomo. Hii itasaidia kuondoa bakteria na mabaki ya chakula kinywani, ambayo yanaweza kusababisha harufu mbaya.

3. Tumia mkusanyiko wa chumvi ya maji ya uvuguvugu kufanya kipigo cha koo - mkusanyiko huu wa chumvi unaweza kupunguza uvimbe na kutoa mabaki ya chakula kwenye koo ambayo yanaweza kusababisha harufu mbaya.

4. Kula vyakula vyenye afya - kula vyakula vyenye protini, mboga na matunda kwa wingi na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari na wanga. Hii itasaidia kupunguza uzalishaji wa mate ya koo na kuzuia kuwepo kwa bakteria kinywani.

5. Kuzuia uvutaji wa tumbaku - uvutaji wa sigara na tumbaku unaweza kusababisha harufu mbaya ya mdomo na kuharibu afya ya koo na mapafu.

6. Pumzika vya kutosha - kupumzika vya kutosha husaidia kupunguza mafadhaiko na kuimarisha mfumo wa kinga.

Kumbuka kuwa ni muhimu kushauriana na daktari wako ikiwa una harufu mbaya ya mdomo inayosababishwa na mate ya koo, kwani hii inaweza kuwa dalili ya shida ya kiafya.

0
Topic starter

Nimeenda kila hospitali ! Mwananyamala , Albert Kairuki, RABININSIA, Almandari posta na pharmacy ndo usisemeee! I’m totally tired of living!😔😔😔😔

0

Una uhakika na hili jibu lako mkuu?umeenda kila hospitali sawa, alafu huwa wanakwambia tatizo ni nini baada ya vipimo? ..
Nilikushauri uonane na specialist au super specialist wa kinywa na meno, ilo pia umeshawai fanya?

0

Almandari ndio hospital gani jomba? Hebu kuwa serious. Au umemega kipande cha nnya bro😀😀😂

0

Dah kumbe sipo pekeangu kama umefanikiwa nijuze dawa na Mimi 

0

Nenda na muhimbili, na pia siku ukisikia madaktari bingwa kutoka nje wamekuja tafadhali kawaone

Bila kusahau jatibu na hizi hospitali za kichina/korea huwa wana matibabu ambayo unaweza kustaajabu kwa mafanikio lakini kwao kawaida sana

0

Pole sana...

0

Pole sana.

Kila Tarehe 27 Mwisho wa mwezi,tunapakia Container kutoka Japan kwenda Dar✅ Lipia mzigo wako mapema week moja kabla ya mzigo kuondo.✅✅👍💪🙏🏿


Digxam

FREE
VIEW